Tuesday, March 11, 2014

Malaysia yazidisha kasi kutafuta Ndege



Ndugu wa waliopotea wameelezwa kuwa wakae tayari kupata habari mbaya
Shughuli ya kutafuta ndege ya abiria ya Malaysia imeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya suitofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea wakiwa katika ndege hiyo.
Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.
Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.

Waasi wa Darfur washambulia wanajeshi



Sudan inalaumu Sudan Kusini kwa kuunga mkono waasi hao
Waasi kutoka jimbo la Darfur nchini Sudan, wameshambulia kambi ya jeshi Kaskazini mwa Kordofan, na kuwaua wanajeshi 5 katika makabiliano makali . Hii ni kwa mujibu wa jeshi la nchi hiyo.
Eneo la Kordofan Kaskazini halijakuwa likishuhudia mashambulizi kutokana na vurugu katika jimbo la Darfur karibu na mpaka na Sudan Kusini.
Sudan Kusini imekana madai kuwa inaunga mkono waasi wa Darfur.
Maelezo zaidi kuhusu mapigano hayo bado hayako wazi, ingawa makabiliano haya yanakuja kabla ya makataa ya kusitisha usafirishaji wa mafuta kutoka Sudan Kusini kutokana na madai ya kuunga waasi mkono.
Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011, chini ya mkataba wa mwaka 2005 wa kukomesha mapigano yaliyodumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, uhusiano kati ya majirani hao wawili umezorota kuhusu mapato ya mafuta na tuhuma kuwa pande zote zinaunga mkono waasi kupiga mwingine.
Waasi waliopigana vita vya Sudan Kusini wakati wa mapigano, walijipata upande wa mpaka wa Sudan baada ya nchi hiyo kujitenga na kisha wakachukua silaha kupigana wakidai kuwa maslahi yao bado hayatimizwi.
Pamoja na makundi matatu ya waasi katika jimbo la Darfur, waliungana na kubuni kikundi cha waasi cha Sudan Revolutionary Front na wamekuwa wakiendesha harakati zao katika maeneo ya Kordofan ya Kusini na Blue Nile, ambayo yanapakana na Sudan Kusini.

Kutana na Daniel Kish: Kipofu aliyejifunza kuona kwa kutumia Sauti.


daniel kish kipofu anayeona

Daniel Kish alipoteza uwezo wake wa kuona tangu akiwa na umri wa miezi 13, kwa ugonjwa wa Saratani.
Kwa kutumia sauti (Clicking Sound)  inayoitoa kwa kugonga ulimi wake kwenye kuta za midomo na kufuatilia Mwangwi wake, Kish anaweza kutambua vitu vyote vilivyo karibu yake. Kish hutumia ujuzi huo ujulikanao kama Echolocation, ambao pia hutumiwa na mnyama Popo “Kuona” na kujua vitu vinavyo mzunguka.
Kwa kutumia ujuzi huo Kish anauwezo wa kundesha baiskeli kwenye barabara za kawaida. Pia anauwezo wa kutambua majengo yaliopo umbali hadi mita 300, kutofautisha aina ya magari na mambo mengine yanayo mwezesha kuishi maisha yake kama mtu anayeona.
Maoni yako