WASANII WANAJUA UMUHIMU WA JUKWAA LA
SANAA?
Nimekuwa nikihudhuria konga mano la
Jukwaa la sanaa kila wiki kama ilivyo pangwa na Baraza la Sanaa
Tanzania(BASATA),kwalengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayo husu sanaa na
wasanii ,pia kwa kupitia Jukwaa hilo nime weza kuwafahamu wadau mbalimbali na
wasanii mbalimbali.
Katika Jukwaa la sanaa kawaida yake
huwa kuna kuwa na mada zilizo andaliwa na wataalamu mbalimbali ambao wanakuwa
wamechanganua nakufika maamuzi ya kuliweka mezani ili wasanii waweze kujifunza
pamoja na wadau wa sanaa waweze kuchangia
madahiyo ambayo inakuwa mezani.
Kama Basata imetambua umuhimu wa
kuanzisha Jukwaa hilo ,na ninaamini kilakitu kinachokuwa kimewekwa basi kina
wekwa kwa malengo maalumu na kina kuwa nasababu maalumu zinazopelekea kuwepo
kwakitu cha namuna hiyo,kwa upande wangu nina ipongeza Basata kwa kuanzaa
programu hiyo kwani maono yangu kwa kupitia Jukwaa hilo wasanii watapata fursa
za kujifunza mambo mbalimbali.
Nakumbuka kuna mada moja ambayo
nilivutiwa nayo sana mada iliyokuwa ikizumzia juu ya ‘’kwa nini watanzania
wengi wanathamini kazi za wasanii wa nje na kudharau au kuto kuthamini kazi
zetu sisi wenyewe tunazo zitengeneza wenyewe kama Muziki na filamu’’
Mada hiyo ilinivutia sana na
waendesha mada waliweza kuichambua vizuri sana,lakini kilicho ni sikitisha
nikwamba walengwa wenyewe hawakuwepo ,jambo lililo nipa maswali mengi na kupata
uchungu kwamba Basata imeandaa mada kwa kuamini au kwa dhumuni kubwa la walengwa
waweze kufikiwa na mada hizo ili kama kunakuwa na vitu vya wasanii kubadirika
basi waweze kufanya kitu chatofauti, nasio kuona mabadiliko katika sanaa yana
baki yaleyale na kusababisha sanaa kuto kukua bali kupotea kabisa.
Idadi ya wasanii kuhudhuria katika
Jukwaa la sanaa imekuwa ndogo sana wakati mwingine hakuna msanii yeyote ambaye
ni maalufu anayeweza kuja jambo ambalo linalo pelekea dhumuni la kuweka Jukwaa
hilo kuto tiliwa maanani, kwani wasanii chipukizi ndio ambao wanahudhulia ,
jambo ambalo wasanii hao chipukizi wanajifunza kutoka kwa wasanii wanao fahamika
namaanisha maarufu.
Kunapotokea matatizo ya sanaa au kazi
ya sanaa kuto kwenda vizuri ambao wanakuwa wamefanya ni hao wasanii.chaajabu
Basata inapoona hayo na kuamua Kuandaa mada ya kuweza kutatua hilo tatizo au
kusikiliza wasanii kama wa sanii wanataka nini ,utaona hawahudhurii katika
Jukwaa la sanaa na kupuuza.
Kinacho nishangaza nikwamba kwenye
vitu mhimu kama hivi vya kujadili mada ukiwahusisha wa sanii hawafiki katika
Jukwaa sijajua nini tatizo la wasanii ni kudharau mada?au nini lakini katika
Maonyesho mengine ambayo sio mhimu uta wakuta wakiwekea kipaumbele.
Wito wangu wasanii ebu tambueni
umuhimu wa kuwa najukwaa hilo kwani ni muhimu na lina faida .kuliko kuendelea
kulalamika na kulaumu pasipo kuja wenyewe kwenye Jukwaa muweze kuchangia hoja
na kujifunza mambo mengine mazuri ya kufanya tasnia yetu ya sanaa isonge mbele.
No comments:
Post a Comment