SANAA YETU INASONGA MBELE AU INAANGAMIA
Sito acha kusahau maneno ya wahenga
wetu kwani walisema (YA KALE NIDHAHABU) wakiwa na maana ya kituchochote cha nyuma ni bora zaidi
kuliko kipya, kwani kuna watu wakiona wamepata kitu kipya basi wana dharau kitu
cha nyuma.,Au kulingana na utandawazi utaona mambo yakale yakiwa mstari wa
nyuma sana na kusahaurika na kuona
hayana maana na kuendeleza mambo ya kisasa na kusahau kabisa ubora wa
mambo ya nyuma.
Msomaji wangu nazungumzia tasnia ya
sanaa toka enzi za miaka ya 79 kurudi nyuma kiukweli tamaduni za asili zilikuwa zina pamba
moto na enzi hizo tulikuwa tunajivunia sanaa yetu ,sio sasa yani kadri siku
zinavyoenda na pata machungu sana ninavyoona asili yetu inapotea siku hadi siku
na kusahau kabisa kama inabidi tuukuze
utamaduni wetu na sio kuacha watu wakautumie utamaduni wetu.
Miaka ya nyuma tukiangalia bendi za
muziki kama sikinde,msondo,resiwanyika
kweli tunaona mashairi yaliyo pangwa kwa vina na ukisikiliza unapata mafunzo
mengi bila kujari unasikiliza na nani. Kiukweli miaka ya nyuma tukizungu mzia
mziki tunayo ya kuzungumza lakini kwa sasa nashidwa nianzie wapi kwani kumekuwa
na miziki ya aina nyingi na kila mziki una staili yake na suala la kitamatuni au
maadili halija wekewa mkazo sana na kudharaulika kabisa.
Nikiangalia hali ya sanaa ya sasa
naona itakuja kufika sehemu suala la utamaduni likapotea kabisa kwani kwa sasa
kila mtu anajaribu kufanya mziki kulingana nay eye anataka nini na si kuangalia
je niwatu gani watakwenda kusikiliza au kuangalia kazi yangu , jambo hilo
linasikitisha sana kwani kuna baadhi ya nyimbo na video za muziki zinapotosha
kabisa ukiangalia kama mtu mzima umekaa na watoto itabidi usimame na kutoka nje
je/ halihiyo inapeleka wapi tamaduni
yetu. Ni tuna kuza au kubomoa?
Kama wasanii ina bidi tufike mahari
na kubadilika na kujalibu kuangalia wapi tuliko toka na wapi tunaenda ili
kuhakikisha kazi zetu zinafika sehemu nzuli na kuweza kufahamika mataifa na
mataifa ,lakini kama utaendeleza kuharibu kwa kufanya sanaa za ajabu kama ngoma
za vigodoro, ngoma za kanga moja na
nyingine zinazo vunja utamaduni hatuta songa mbele na tutaibua tamaduni
nyingine ni mhimu kutunza tamaduni zetu. Msomaji kwaleo ni hayo tuu panapo
majariwa tutaendelea
No comments:
Post a Comment