MANUFAA YA BIMA KWA
WASANII
Na AGNES MHAGAMA
Kwakupitia
programu ya kila wiki Baraza la sanaa (BASATA) limetoa elimu
kwa wadau wa sanaa na wasanii kuhusu umuhimu wa kuwa na bima kwa ajiri
ya ulinzi wa afya zao pamoja na mali zao.
Hayo yamebainishwa na
Afisa masoko wa
kampuni ya MGEN inayojishughulisha na
mambo ya bima na Bw.JAFARRY JUMBE wakati akiongea na wasanii pamoja na wadau wa
sanaa katika Jukwaa la sanaa jijini Dar es salaam.
Bw.jumbe alisema wasanii watafaidika na huduma hiyo popote watakapo kama
vile,msanii akipata matatizo ya ajali, kuungua kwa mali zake, kupatwa na
maradhi , kama kampuni ya MGEN itahusika na ulipaji wote wa awali wa mali yake.
Aliongeza kwamba, msanii kuwa na bima ni mhimu kwani katika
kazi zake za kukuza sanaa anakumbana na changamoto mbalimbali kwahiyo kama atakuwa na Bima ita msaidia yeye kuweza
kufidia baadhi ya sehemu atakazo kuwa ameshindwa kutekeleza.
Hatahivyo alisema kampuni imeamua kugawa bima kwa ngazi mbalimbali ilikulahisisha kila mtu aweze kuwa na bima
mojawapo kama bima ya mtu mmoja, bima ya vikunndi vya watu
,bima ya mali ,ili kumsaidia msanii
aweze kuwa na bima itakayo msaidia katika ulinzi wa mali zake kwa haraka zaidi.
Licha ya hayo aliwataka wasanii kutokuwa na hofu ya gharama na kuepuka maneno ya mitaani yanayo toa taarifa za uongo juu ya huduma hiyo kwani kampuni hiyo imeweza kuweka
gharama ndogo zitakazo mfanya mtu yoyote aweze kukidhi.
No comments:
Post a Comment