WASANII WA SARAKASI WA ILALAMIKIA SERIKARI
Kampuni ya Simple Entertainment inayo jishughulisha na kuinua vipaji
vya sarakasi ndani ya nchi na nje ya
nchi imeiomba serikari kutupia jicho
sanaa hiyo kwani imekuwa ikisahaulika na
kutothamini wa katika sanaa hiyo,licha ya kuwa imekuwa ikifanya kazi kubwa ya mchango wa kuitambulisha nchi na kutangaza katika mataifa mbalimbali duniani.
Hayo yamezungumzwa hivi karibuni
na mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Jacob Chinunda, wakati akizungumza
na wasanii pamoja na wadau wa sanaa
katika kongamano la kila wiki la jukwaa la sanaa linaloendeshwa na Baraza la sanaa la taifa (BASATA)
jijini Dar es salaam.
Chinunda alisema sanaa ya sarakasi ina bidi ithaminiwe na kuwekewa
mkazo kama sanaa nyingine , kwani ni sanaa ya kipekee ambayo imekuwa
ikitambulisha nchi katika mataifa mbalimbali kupitia maonyesho ambayo wanakuwa
wakifanya, kutokana na soko dogo la nchi yetu na kutothaminiwa sanaa
hiyoimekuwa ikifanya na kuchezwa kila mara nje ya nchi kwa lengo la kutafuta
masoko na kupendwa zaidi na watu wa nje ya nchi.
“wasanii wa sarakasi wamekuwa wakipata shida nyigi katika kupata ma
agence kwani kwa nchi yetu ni wachache
sanaa ,mpaka uwe agence nilazima uwe msanii wa sarakasi,kadri siku zinavyo zidi
kwenda wasanii hao wamezidi kupotea na kukatatamaa ya sanaa hiyo kulingana na
changamoto wanazo kumbana nazo”alisema.
Aliongeza kwamba, sanaa hiyo imekuwa ikitambulisha vizuri jina la Tanzania
kwani kila wanapotaka kufanya onyesho ni lazima upeperushe bendela ya nchi yako ikiwa ni
utambulisho wa sehemu uliyo toka,hali hiyo imepelekea kwa watalii wengi kupenda
kuja Tanzania kwa ajili ya kujionea maonyesho hayo ya aina yake.
Licha ya hayo alieleza
changamoto wanazo kumbana nazo ikiwemo na serikali kuwasahau kwani imepelekea
sanaa hiyo kuto endelea na kufahamika zaidi kimataifa na dunia nzima kama
ikiwemo usumbufu mkubwa wanapokuwa wanasafiri,wanapokuwa wanataka bendera ya
taifa imekuwa nitatizo kwani hadi ina wa
gharimu kutafuta vitambaa na kutengeneza bendea li iweishara ya utambulisho wan
chi wanayotokea.
No comments:
Post a Comment