Wednesday, June 24, 2015

WAJUA??TAIFA QEENS KIHUNZI NAMIBIA


Taifa Queens itaruka kihunzi Namibia?

wachezaji wa netball wa Tanzania.
Chama cha netball Tanzania (Chaneta) kimesema kina imani timu ya taifa, Taifa Queens itapeperusha vema bendera ya nchi hiyo katika michuano ya Afrika itakayofanyika nchini Namibia June 28.
Timu hiyo inategemewa kukabidhiwa tiketi Jumatano tayari kwa safari ya kuelekea Windhoek, Namibia kati ya Alhamisi au IJumaa wiki hii, kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa Chaneta, Anna Kibira.
Kiongozi wa chama cha mchezo huo Tanzania Bara (Chaneta), Anna Kibira amesema kuwa watachagua timu kwa kushirikiana na wenzao wa Zanzibar (Chaneza) kwa ajili ya kuanza kambi hapo Mei 17 visiwani Zanzibar.
Tanzania iliombwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kabla ya kuhamishiwa Namibia, lakini imeshindwa kutokana na uhaba wa fedha.Awali, Zambia iliteuliwa kuwa mweyeji kabla ya Tanzania kuombwa na ilishindwa kwa sababu kama hizo.
Tanzania ilishindwa kushiriki michuano hiyo ya mwaka 2013 iliyofanyila Blantyre, Malawi kutokana na ukosefu wa fedha , lakini Kibira amesema watafanya jitihada ili kuhakikisha wanasafiri kwenda Namibia kushiriki. Nchi mbalimbali za Afrika kama vile Kenya, Uganda zinategemewa kushiriki michuano hiyo.


FAHAMU NINI KIMEJILI KATIKA MICHEZO


Liverpool yamsajili Firmino wa Brazil

Na, Agnes mhagama

Liverpool imesajili mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino
Klabu ya Liverpool imemsajili mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino kutoka klabu ya Hoffenheim kwa kanadarasi ya miaka mitano itakayogharimu pauni millioni 29.
Mkataba huo utaandamana na ukaguzi wa kimatibabu ambao utafanyika baada ya mchezaji huyo kurudi kutoka Chile ambapo amekuwa akiichezea Brazil katika michuano ya Copa America.
Firmino ambaye amefunga mabao 47 katika mechi 151 akiwa katika kilabu ya Hoffenheim atakuwa mchezaji wa pili wa Liverpool aliyeghali mno.
Kilabu hiyo ya Anfield ilimfanya mchezaji Andy Carroll kuwa mchezaji ghali alipojiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 35 kutoka Newcastle mwaka 2011.

HABARI, SIMULIZI NA MATUKIO MBALIMBALI

 Wapenzi wasomaji wa safu hii ya blogsport napenda niombe radhi kwa kpindi kikubwa nilipo kuwa kmya ,kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wangu .nitumie nafasi hii kuwa karibisha tena na tena kwani nimejibanga kikamilifu kuwaleteeni matukio malimbali na simulizi mbalimbali zenye kujenga na kusisimua , pia utaweza kuona picha mbalimbali katika matukio mbalimbali,
lakini pia unapata nafasi ya kuweza kunitumia maoni yako na mchango wako ili tuweze kwenda sambamba


                                KARIBUNI SANAAA! BY AGNES MHAGAMA JOURNALIST