Thursday, May 21, 2020

DAWA YA MALARIA JE INATIBU CORONA?

Jaribio la matumizi ya dawa za malaria kuona kama zinaweza kuzuia ugonjwa wa Corona limeanza nchini Uingereza katika mji wa Brighton na Oxford.
Chloroquine, hydroxychloroquine au placebo zitatolewa kwa wafanyakazi wa afya zaidi ya 40,000 kutoka Ulaya, Afrika, Asia na Amerika ya kusini.
Washiriki wote ni watumishi wa afya ambao wanahudumia wagonjwa wa Covid-19.
Rais Donald Trump alikosolewa baada ya kusema kuwa ametumia dawa ya malaria iitwayo hydroxychloroquine, licha ya angalizo kuwa inawezekana si salama kutumia dawa hiyo kwa ajili ya corona.
Mshiriki wa kwanza, Uingereza katika jaribio la kwanza la kimataifa imesema siku ya Alhamisi katika hospitali ya Brighton na hospitali ya chuo kikuu cha Sussex pamoja na hospitali ya John Radcliffe mjini Oxford.
Watapewa dawa ya hydroxychloroquine au placebo kwa kipindi cha miezi mitatu.
Wakati Asia, washiriki watapewa chloroquine au placebo.
Mipango ya awali ni katika majimbo 25 ya Uingereza na matokeo yanatarajiwa mwishoni mwa mwaka.
Jaribio hilo liko wazi kwa yeyote ambaye anatoa huduma moja kwa moja kwa wagonjwa wenye virusi vya corona nchini Uingereza, ikiwa kama bado hawajapata maambukizi ya virusi vya corona.
Jaribio hili litaangalia kama dawa hizo zitaweza kuzuia wafanyakazi wa afya kupata maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa wagonjwa.

'Ina manufaa au ni hatari'

Utafiti mmoja wa Prof Nicholas White kutoka chuo kikuu cha Oxford alisema: "Kiukweli hatufahamu bado kama chloroquine au hydroxychloroquine kama ni kinga au zina madhara dhidi ya Covid-19."
Lakini alisema, utafiti wa maeneo mbalimbali kama huu , ambapo si mshiriki au mtafiti anafahamu kuwa kupewa dawa hiyo ndio namna nzuri ya kujua umuhimu wa dawa husika.
"Chanjo ambayo ni salama na yenye uhakika itachukua muda mrefu kupatikana," alisema Prof Martin Llewelyn kutoka Brighton na chuo cha afya cha Sussex, ambaye pia anaongoza utafiti huo.
"Kama dawa za malaria za chloroquine na hydroxychloroquine zinaweza ,kupunguza urahisi wa mtu kuambukizwa virusi vya corona, basi itakuwa jambo bora zaidi ambalo litasaidia."
Dawa hizo zinaweza kupunguza homa na maambukizi na kuweza kutumika pia kwa ajili ya kuzuia na kutibu malaria.
US President Donald Trump speaking at the White HouseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Trump alizungumzia kabla kuhusu matumizi ya dawa hizi kwa ajili ya Covid-19
Kituo cha kujitolea cha Lupus nchini Uingereza na Marekani kimetoa wasiwasi wake kuhusu ongezeko la uhitaji wa dawa hiyo kwa ajili ya virusi vya corona kunaweza kuhatarisha hali za wagonjwa ambao wanazitegemea tayari, kama zitapungua wagonjwa wa malaria watapata shida kuzipata ili kutibiwa.
Dawa hizo zimepata umaarufu baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa dawa hizo zinaweza zikasaidia katika janga hili la corona, na wiki hii alitumia dawa ya hydroxychloroquine ili kujizuia kupata maambukizi ya corona.
Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani ilitoa angalizo dhidi ya matumizi ya dawa hizo nje ya hospitali, wakati wakitoa ruhusa ya dawa hizo kutumika katika kesi kadhaa au majaribio ya kitabibu.
Wakati chuo kikuu cha Oxford kikifanya jaribio la kuzuia maambukizi katika mazingira ya huduma za afya, shirika la afya duniani limetoa angalizo kuwa baadhi ya watu ambao wanajitibu wenyewe wanaweza kupata madhara makubwa.
Hazijaonekana kuwa salama na zenye uhakika wa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona bali kuna hatari ya kupata matatizo makubwa ya moyo.
Utafiti huo umejumuisha watafiti kutoka Uingereza, Thailand, Vietnam, Laos, Cambodia na Italia.


No comments:

Post a Comment