Saturday, July 16, 2016

LEO WATANZANIA MACHO YOTE KWA YANGA

TIMU ya Yanga leo inatupa karata yake muhimu katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwakaribisha Medeama FC ya Ghana, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inayoshika mkia kwenye kundi lake la A, na inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kurudisha matumaini ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa upande wa klabu barani Afika.
Kocha wa Yanga, Hans Pluijm amesema jeshi lake lipo tayari kwa ajili ya mchezo huo huku akijivunia kurejea kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe, aliyeukosa mchezo uliopita kutokana na kuwa na kadi mbili za njano alizozipata kwenye michezo iliyopita.
Uwepo wa Tambwe ni wazi utaongeza ukali wa safu ya ushambuliaji, ambayo haijafunga hata bao moja katika mechi mbili zilizopita ambazo zote wamepoteza mbele ya MO Bejaia na TP Mazembe na kuifanya timu hiyo iburuze mkia kwenye kundi lake.
Pluijm alisema amekiandaa kikosi chake kucheza kwa kushambulia zaidi ili kuhakikisha wanapata mabao mawili ya haraka kwenye kipindi cha kwanza ili kuwavunja nguvu wapinzani wao Medeama ambao wamekuja nchini wakiwa na matumaini ya kuvuna pointi tatu.
Mholanzi huyo alisema anataka kuiona timu yake ikicheza eneo la wapinzani wao kwa sehemu kubwa ya mchezo jambo ambalo litawarahisishia kupata bao muda wowote hasa kutokana na mpango wa kutumia washambuliaji watatu kwenye mchezo huo.
“Ukweli huu ni mchezo muhimu kwetu lazima tushinde ili ndoto zetu za kucheza nusu fainali ziweze kutimia ndiyo sababu tumejipanga vizuri katika muda tulioupata baada ya kucheza na TP Mazembe na ninafurahi kuona wachezaji wangu wote wapo katika hali nzuri na wanajua umuhimu wa ushindi katika mchezo huo,”alisema Pluijm.
Pluijm alisema anajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na Medeama nao kuhitaji ushindi, lakini atahakikisha wanaitumia vizuri nafasi ya kucheza nyumbani kupata ushindi ili pia kuwafurahisha mashabiki wao ambao waliwaangusha katika mchezo uliopita kwa kufungwa na TP Mazembe.
Alisema baada ya kupoteza michezo miwili iliyopita wasingependa kupata matokeo hayo kwa sababu mipango yao ni kuhakikisha wanaanza kushinda mchezo huo na mingine iliyobaki ili kutimiza kile walichokipanga.
Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo akiziba nafasi ya Kelvin Yonda ambaye hatocheza mechi hiyo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano, lakini pia kiungo Deusi Kaseke huenda asicheze kutokana na kuwa majeruhi baada ya kupata ajali ya piki piki siku za karibuni.
Kocha wa Medeama Prince Yaw Owusu, ametamba kuwa amekuja Tanzania kuchukua pointi tatu ili waweze kufufa matumaini ya kucheza hatua ya nusu fainali. Owusu, alisema anawajua vizuri wenyeji wao Yanga, na haoni kitu ambacho kinaweza kumzuia asipate ushindi kutokana na kikosi chake kuwa katika kiwango cha juu hivi sasa baada ya kufanya vizuri kwenye mechi za ligi ya Ghana.
“Najua mchezo utakuwa mgumu lakini kuijua kwangu Yanga kutasaidia kupunguza presha kwa wachezaji wangu ambao naamini hakuna anayeijua Tanzania wala Yanga yenyewe, lakini tumekuja tukihitaji pointi tatu na nina hakika wa kuzipata kwa sababu katika timu nyepesi kwenye kundi letu basi ni hii,”alisema kocha huyo.
Owusu alisema kikosi chake kitaingia uwanjani kikiwa kinawategemea zaidi viungo wa

No comments:

Post a Comment